728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 13, 2016

    MEDEAMA FC YAIKANA TP MAZEMBE MCHANA KWEUPE

    Accra,Ghana.

    Klabu ya Medeama FC ya Ghana inayoshiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika imekana kupokea ofa toka Klabu ya TP Mazembe ya Congo DR kwa ajili ya kumuuza Kiungo wake tegemeo Malik Akowuah,26.

    Medeama FC kupitia kwa Mtendaji wake Mkuu,James Essilfie,imekana kata kata kupokea ofa toka TP Mazembe na kuziita taarifa hizo kuwa ni uzushi mtupu.

    Essilfie amesema "Taarifa hizo ni uzushi.Kweli TP Mazembe wameonyesha kuvutiwa na mchezaji wetu lakini mpaka sasa bado hawajafanya mawasiliano yoyote na sisi.

    "Hawajatuma ofa kwa ajili ya kutaka kumsajili Malik,lakini kama watatuma basi tutaweka wazi kila kitu/tutawaambieni"Alimaliza Essilfie.

    Ikiwa uhamisho huo utafanikiwa, Malik atakuwa ni Mghana wa tano kujiunga na TP Mazembe.Wengine ni Daniel Nii Adjei, Gladson Awako, Richard Kissi Boateng,Yaw Frimpong na Solomon Asante.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MEDEAMA FC YAIKANA TP MAZEMBE MCHANA KWEUPE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top