728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 12, 2016

    AZAM TV YABORESHA ZAWADI LIGI KUU,TIMU KUPATA ZAWADI KULINGANA NA NAFASI

    Dar es Salaam,Tanzania.

    Mkataba mpya wa Azam Media kurusha matangazo Live ya Ligi Kuu Bara utagharimu Sh bilioni 23.

    Mkataba wa awali, kila klabu ilikuwa inapata Sh milioni 100 kwa msimu lakini sasa itaingiza karibu mara mbili ya hizo.

    Katika mkataba uliosainiwa leo, klabu itapata Sh milioni 42 kwa mafungu matatu ambayo ni Sh milioni 126.

    Fungu la mwisho la milioni 42 litatolewa kwa mfumo tofauti ambao utakuwa hivi.

    Timu inayoshika nafasi ya juu katika msimamo inafaidika kwa kupata zaidi na itakwenda hivyo hadi chini.

    Maana yake ligi itakapoisha, zitazokuwa
    juu kimsimamo zitapata fedha nyingi zaidi na zilizo chini zitaendelea kusota
    kwa kupata kiduchu.

    Lengo kuu ni kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa kila kikosi kuona umuhimu
    wa kukaa juu katika msimamo wa ligi hali itakayochangia ushindani uwanjani kwa kila timu kutaka kushinda karibu
    kila mechi ili mwisho wa ligi ifaidike.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AZAM TV YABORESHA ZAWADI LIGI KUU,TIMU KUPATA ZAWADI KULINGANA NA NAFASI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top