Cairo,Misri.
Waamuzi kutoka Misri ndiyo watakaochezesha mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga
na Medeama ya Ghana itakayochezwa Julai 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Ibrahim Nour El Din kuwa mwamuzi wa kati kwenye mechi hiyo wakati waamuzi wasaidizi ni Ayman Degaish na Samir Gamal Saad.
Mohamed Maarouf Eid Mansour atakuwa mwamuzi wa akiba. Waamuzi wote ni raia wa Misri.
Raia wa Zambia,Pasipononga Liwewe
atasimama kama kamisaa, Mfubusa Bernard kutoka Burundi atakuja kama mkaguzi wa waamuzi huku Ian Peter Keith Mc Leod kutoka Afrika Kusini ndiye mratibu mkuu wa pambano.
0 comments:
Post a Comment