Napoli,Italia.
MSHAMBULIAJI wa Ufaransa,Olivier Giroud yuko tayari kuachana na klabu yake ya Arsenal katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Hii ni kwa mujibu wa wakala wake, Michael Manuello.
Kauli hiyo ya Manuello imekuja baada ya Arsenal kuripotiwa kuwa na mpango wa kumfanya Giroud,29, chambo katika mbio za kuiwania saini ya mshambuliaji wa Napoli,Muargentina,Gonzalo Higuain.
Taarifa kutoka nchini England na Italia zinadai kuwa Arsenal imeanza mazungumzo na Napoli kwa ajili ya kuangalia uwezo wa kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo Gonzalo Higuain.
Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa Arsenal imedaiwa kuwa tayari kumtoa Giroud pamoja na Paundi Milioni 42 ili kumsajili Higuaini ambaye msimu uliopita alikuwa mwiba mkali Italia baada ya kufunga mabao 36 katika michezo 38 ya Seria A.
Manuello amesema mteja wake (Giroud) hatakuwa kikwazo kwa Arsenal kumpata Higuaini na ameongeza kuwa Giroud hana hofu ya kuhamia Napoli na ana amini kuwa mfumo unaotumiwa na Kocha wa klabu hiyo, Maurizio] Sarri ,unaweza kuongeza makali ya mshambuliaji huyo.
"Kwa sasa Giroud ni mchezaji wa Arsenal.Hatujawa katika mazungumzo na Arsenal wala Napoli.Lakini Arsenal wakituambia ondokeni,tutaondoka."Alikaririwa Manuello.
0 comments:
Post a Comment