California,Marekani.
MABAO mawili ya kila kipindi yameiwezesha Mexico kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Copa America Centenario baada ya kuifunga Jamaica mabao 2-0 katika mchezo wa pili wa kundi C ulioisha hivi punde katika uwanja wa Rose Bowl,California.
Mexico ilipata bao lake la kuongoza dakika ya 18 tu ya kipindi cha kwanza baada ya Javier Hernandez "Chicharito"kufunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Jesus Corona.
Dakika ya 81 Oribe Perlata aliiandikia Mexico bao la pili baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa kiungo Hector Moreno na kufumua mkwaju uliomshinda kipa wa Jamaica,Andre Blake na kutinga wavuni.
Kwa matokeo hayo Mexico na Venezuela zimefuzu robo fainali huku Jamaica na Uruguay zikiaga baada ya kupoteza michezo yao miwili ya kwanza.
VIKOSI
MEXICO
13Guillermo Ochoa
3Yasser Corona
2Néstor Araújo
15Héctor Moreno
20Jesús Dueñas
4Rafael Márquez
7Miguel Layún
16Héctor Herrera
14Javier Hernández
10Jesus Corona
9Raúl Jiménez
JAMAICA
1 Andre Blake
4Wes Morgan
19Adrian Mariappa
21Jermaine Taylor
15Je-Vaughn Watson
16Lee Williamson
3Michael Hector
10Jobi McAnuff
22Garath McCleary
8Clayton Donaldson
9Giles Barnes
0 comments:
Post a Comment