Manchester, England.
Paul Scholes amevitazama vilabu vya England katika michuano ya ligi ya mabingwa wiki hii na kusema ligi ya nchi hiyo kwasasa siyo bora tena na kuongeza Sergio Aguero ndiye mchezaji pekee anayeweza kupata namba katika vilabu vya Real Madrid,Barcelona na Bayern Munich kutoka ligi ya EPL.
Scholes ambaye kwasasa ni mchambuzi wa masuala ya soka ameibuka na kauli hiyo kufuatia mwenendo mbaya wa vilabu vya England katika michuano inayoendelea ya ligi ya mabingwa barani Ulaya na kusisitiza kuwa kinachoishusha ligi hiyo ni vilabu kuendelea kusajili wachezaji wa kawaida kinyume na vilabu vya nchi nyingine ambavyo vinashindana kusajili wachezaji mahiri.
Scholes Ameongeza kuwa vilabu vya England vimepigwa bao kwa sehemu kubwa na vilabu vya Real Madrid,Barcelona,Bayern Munich na hata Juventus na Paris Saint Germain.
"Wachezaji wote wazuri wako Hispania na Ujerumani na kidogo Italia na Ufaransa.Hawaji England.Kutoka England ni Sergio Aguero pekee ndiye mwenye uwezo wa kucheza Real Madrid,Barcelona na Bayern Munich.Hii ni kutokana na ubora alionao"
0 comments:
Post a Comment