Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski ameendelea kuonyesha kuwa msimu huu amekuja kivingine baada ya kuendelea kufunga kila aonapo lango la adui liko mbele yake.
Ukali wa Lewandowski umeendelea kujidhihirisha hivi karibuni baada ya kufunga magoli matano ndani ya dakika tisa dhidi ya Wolfsburg katika ligi ya Bundesliga kisha kufunga mengine mawili dhidi ya Mainz O4 na kufunga kazi siku ya jumanne kwa kufunga magoli matatu (hat-trik) dhidi ya Dynamo Zagreb katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya na kumfanya mshambuliaji huyo raia wa Poland kuwa na jumla ya magoli kumi katika michezo mitatu tu na hivyo kuwa mshambuliaji mwenye magoli mengi zaidi ya washambuliaji wengine toka ligi tano kubwa za Ulaya za Ujerumani,England,Hispania,Italia na Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment