Vilabu vya Liverpool,Tottenham Hotspurs na Celtic vimeendelea kuonyesha kuwa safari hii Uingereza ina wakati wakati mgumu sana katika michuano ya Ulaya baada ya kulazimishwa kwenda sare katika michezo yao ya jana usiku ya ligi ya Europa.
Liverpool iliyokuwa nyumbani Anfield imeshindwa kuifunga FC Sion ya Uswisi na kutoka nayo sare ya goli 1-1.
Liverpool ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli dakika ya 4' tu ya mchezo kupitia kwa Adam Lallana akiunganisha pasi safi ya Divock Origi.Kuingia kwa goli kuliiamsha FC Sion iliyokuja juu na kufanikiwa kupata goli zakika ya 18' kupitia Ebenezer Assifuah.
Katika mchezo mwingine Tottenham Hotspurs ilishindwa kulinda goli lake la dakika ya 8 la kiungo Erik Lamela na kuambulia sare ya goli 1-1 na AS Monaco iliyosawazisha dakika ya 81 kupitia kwa Stephan El Shaarawy.
Matokeo mengine ya Europa ligi haya hapa....
Basel 2-0 Lech Poznan
Belenenses 0-4 Fiorentina
Lazio 3-2 Saint-Etienne Napoli 2-0 Legia Warsaw
Viktoria Plzen
Rapid Vienna1-0 Dinamo Minsk.
Celtic 2-2 Fenerbhace
FC Krasnodar 2-1 Qabala
PAOK 1-1 Borussia Dortmund
Qarabag 1-0 Anderlectch
0 comments:
Post a Comment