728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, October 02, 2015

    KUMEKUCHA:ARSENAL YAINGIZA NYOTA WAWILI KINYANG'ANYIRO CHA TUZO YA BALLON D' OR MWAKA HUU,BARCA,MADRID ZATOA 14

    Barcelona,Hispania

    TAYARI.Gazeti la Mundo Deportvio la Catalunya,Hispania leo ijumaa limetoa orodha ya wachezaji 59 wanaotarajiwa kuingia katika kinyang'anyiro cha kumsaka mchezaji bora wa mwaka wa dunia.

    Katika orodha hiyo inayotarajiwa kupunguzwa na kubaki na wachezaji 23 na kisha kumpata mshindi mmoja,klabu ya Arsenal ambayo imeendelea kuvurunda kwenye michuano ya Ulaya imeingiza nyota wawili katika kinyang'anyiro hicho kikubwa zaidi dunia.

    Wachezaji hao ni Alexis Sanchez na David Ospina ambao walijiunga na klabu hiyo ya London msimu uliopita wakitokea vilabu vya Hispania na Ufaransa.Sanchez ameingia katika orodha hiyo baada ya kuibuka mfungaji bora wa Arsenal kwa msimu uliopita na kisha kuisaidia Chile kutwaa kombe la Copa Amerika mwezi julai mwaka huu huku David Ospina mbali ya kufanikiwa kuwa kipa chaguo la kwanza Arsenal baada ya kumpiku Wojciech Szczęsny pia alifanikiwa kufanya vizuri na Colombia katika michuano ya Copa Amerika huku Chile.

    Wakati huohuo vilabu vya Hispania vya Barcelona na Real Madrid vimeendelea kutamba katika kinyang'anyiro hicho baada ya kutoa wachezaji saba kila kimoja.

    Kutoka FC Barcelona:Claudio Bravo, Javier Mascherano, Andres Iniesta, Lionel Messi, Ivan Rakitic, Neymar na Luis Suarez.

    Kutoka Real Madrid: Gareth Bale, Karim Benzema, Sergio Ramos, Cristiano Ronaldo, Luka Modric, James Rodriguez na Toni Kroos.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUMEKUCHA:ARSENAL YAINGIZA NYOTA WAWILI KINYANG'ANYIRO CHA TUZO YA BALLON D' OR MWAKA HUU,BARCA,MADRID ZATOA 14 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top