Kesi inayomkabili kipa wa Mbeya City, Juma Kaseja dhidi ya klabu ya
Yanga imeahirishwa hadi mwishoni mwa mwezi ujao.
Kesi hiyo inayosikilizwa katika Mahakama ya Kazi Kitengo cha Usuluhishi
imeshindwa kusikilizwa baada ya kutokuwa na umeme.
Yanga inamshitaki Kaseja kwa madai ya kukiuka mkataba wake, kushindwa
kwenda kazini bila ya taarifa jambo ambalo lilikuwa ni kinyume na makubaliano
yao.
Kutokana na tatizo hilo ambalo sasa ni nchi nzima baada ya Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco) ambalo limekuwa halina uhakika na mambo mengi
kutangaza linafanya marekebisho kupitia mtambo wa Kinyerezi jijini Dar es
Salaam.
Tanesco imetangaza siku moja tu kabla ya kukata umeme, jambo ambalo
limeleta usumbufu mkubwa kwa wakazi na wateja wake.
Kutokana na hali hiyo, kazi sehemu mbalimbali zikiwemo katika ofisini za
serikali na binafsi zimesimama kabisa ingawa bado wachumi hawajaeleza kwamba
taifa litaingiza kiasi gani kutokana na hatua hiyo.
Sasa kesi ya hiyo ambayo Yanga ni mlalamikaji na Kaseja ni mshitakiwa
itasikilizwa mwezi ujao mwishoni, matarajio yakiwa Tanesco watakuwa wamerudisha
umeme mambo yaende kama yanayotakiwa.
NA SALEH ALY
0 comments:
Post a Comment