Bin Hussain akiwa na Sepp Blatter |
Mwanamfalme wa Jordan Ali Bin
Al-Hussain ametangaza kuwa atasimama kuwania nafasi ya Urasi wa
Shirikisho la kandanda duniani FIFA kurithi nafasi ya Rais wa sasa
anayestaafu Sepp Blatter.
Wakati wa uzinduzi wa kampeni zake mwanamfalme huyo aliahidi
kufanya mageuzi katika uongozi wa soka,kupambana na rushwa na kuimarisha
soka la wanawake.Alipoteza ushindi mwezi Mei ambapo Sepp Blatter
alishinda kabla ya kutangaza kujiuzulu wadhifa huo.
Maafisa wa ngazi ya juu ya FIFA wanatuhumiwa kuhusika na rushwa na mamlaka za Marekani mapema mwaka huu.
Rais
wa shirikiso la soka barani Ulaya Uefa Michel Platini na Chung
Mong-joon wa Korea Kusini kwa pamoja wameonesha nia yao kuwania nafasi
hiyo ambao uchaguzi wake utakua mwezi Februari mwaka 2016.
0 comments:
Post a Comment