KOCHA wa zamani wa Yanga SC,
Mbelgiji Tom Saintfiet amemfukuza kabisa mshambuliaji wa Tottenham, Emmanuel
Adebayor katika timu ya taifa ya Togo.
Saintfiet aliyeipa Yanga SC ubingwa
wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 2012, ambaye sasa anaifundisha Togo, amesema
hatamuita tena kikosini Adebayor baada ya kukataa wito wa kujiunga na kikosi
kilichomenyana na Djibouti mwishoni mwa wiki katika mchezo wa kufuzu
Fainali za Mataifa ya Afrika.
Na hiyo inakuja baada ya mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 31 kutemwa katika kikosi cha wachezaji 25 wa
-Tottenham watakaocheza Ligi Kuu ya England msimu huu.
Saintfiet amesema; "Kama
unatoka na mwanamke ambaye hana majibu sahihi, unapaswa kutaafuta mwanamke
mwingine,"amesema Saintfiet ambaye ameshangaa Adebayor kushindwa
kutuma hata meseji au email kujibu wito wake timu ya taifa.
Adebayor alicheza na kufunga bao
katika mchezo wa kwanza kufuzu AFCON dhidi ya Liberia Juni na hiyo ilikuwa mara
yake ya mwisho, kabla ya kusema amesikitishwa na kitendo cha Saintfiet
kumpokonya Unahodha.
0 comments:
Post a Comment