728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 09, 2015

    MMEMSIKIA?:ANELKA AVUNJA UKIMYA JUU YA UBUTU WA GIROUD


    Dubai

    Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Mfaransa Nicholas Anelka ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya Mumbai City FC ya India ameibuka na kumkingia kifua mshambuliaji Oliver Giroud na kusisitiza kuwa kitendo cha Arsene Wenger kutosajili mshambuliaji mpya klabuni hapo kinapaswa kiheshimiwe kwani anaamini Giroud ataifanyia makubwa miamba hiyo ya London licha ya ubutu alionao kwa sasa.

    Anelka ambaye aliichezea Arsenal mwaka 1997-98 na kutwaa mataji mawili ya FA na moja la ligi kuu amesema 

    “Arsene Wenger alifanya hivyo pia kwangu - wakati Ian Wright yupo,hakununua mshambuliaji mwingine hivyo ilinipasa kufanya kazi kwa bidii,” 

    “Aliniamini na nikaanza kucheza mara kwa mara na kufanya vizuri.Amefanya uamuzi huohuo kwa Giroud.Wenger anakiamini kikosi chake ndiyo maana hajatumia pesa.

    Anaamini Giroud atafunga magoli mengi ambayo tayari ameshaanza kuyafunga.Ukitazama takwimu zake ni nzuri siyo mbaya.Arsenal ilitwaa taji msimu uliopita na msimu mmoja nyuma sasa kwanini ishindwe sasa?

    “Watu wanapaswa kusubiri mpaka mwisho wa msimu na kisha kuongea kama hakutakuwa na chochote kitakachokuwa kimefanyika.Alimaliza Anelka ambaye pia amewahi kuvichezea vilabu vya Real Madrid,PSG,Manchester City,Bolton Wanderous na Chelsea.

    Giroud amejikuta akipata wakati mgumu toka kwa mashabiki wa Arsenal kutokana na kushindwa kufikia matarajio ya wengi katika upachikaji mabao licha ya kuifungia klabu hiyo mabao 42 katika michezo 101.

     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MMEMSIKIA?:ANELKA AVUNJA UKIMYA JUU YA UBUTU WA GIROUD Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top