728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 10, 2015

    REAL MADRID YATAJA BEI YA CRISTIANO RONALDO.


    Madrid,Hispania.

    Kama unadhani Cristiano Ronaldo hauziki basi andika umeumia.Hakuna mchezaji asiyeuzika duniani ili mradi tu dau sahihi limefikiwa.

    Sasa sikia hii.Rais wa Real Madrid FLORENTINO PEREZ amesema Cristiano Ronaldo anauzika ikiwa tu dau la €1bn (£725m) litawekwa mezani pake na yeye bila kuchelewa atamuachia nyota huo aondoke zake.

    Perez ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo cha redio cha Cadena Cope cha Hispania kufuatia kuibuka kwa habari kuwa muda mfupi kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili PSG ilituma ofa ya €150m (£109m) ili kumsajili Cristiano Ronaldo.

    Perez amesema "Hapa Hispania ni tofauti na nchi kama England,Kila mchezaji hapa ana bei yake kwenye mkataba wake.Hivyo ukitaka kumnunua mchezaji yoyote ni lazima ufikie bei iliyoko kwenye mkataba wake.

    Kwa suala la Ronaldo ni €1bn (£725m) na siyo vinginevyo.Ukishindwa kutoa dau hilo ina maana hutaki kumnunua.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: REAL MADRID YATAJA BEI YA CRISTIANO RONALDO. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top