Mlinzi wa FC Barcelona Muhispania Gerard Pique amekata kuiomba radhi Real Madrid kufuatia kutoa kauli chafu aliyoitoa dhidi ya miamba hiyo ya Santiago Bernabeu.
Pique ambaye mwanzoni mwa wiki hii alijikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na mashabiki wa Real Madrid wakati akiitumika Hispania katika kinyang'anyiro cha kusaka tiketi ya michuano ya Euro 2016 amesema hatishwi na zomea zomea hiyo na kusisitiza kuwa ataendelea kuiombea mabaya Real Madrid.
Amesema "Sijutii chochote kutoa katika kila neno nililosema,nitarudia kuongea mabaya zaidi ya mara elfu.Ndivyo nilivyo,nataka Real Madrid waendelee kufanya vibaya.Huo ndiyo uhasama wa soka ambao umekuwepo Hispania.Acha mashabiki waendelee kunizomea,kitu cha mwisho kitakuwa ni kuachana na timu ya taifa.Alimaliza Pique
Mapema mwezi juni Gerrard Pique aliitolea maneno ya kashfa Real Madrid baada baada ya klabu hiyo kushindwa kutwaa taji lolote huku yeye na klabu yake ya FC Barcelona wakitwaa mataji matatu.
Kufuatia kitendo hicho mashabiki wa Real Madrid wamekuwa wakimuandama Pique kwa kumzomea na kumchafua katika mitandano ya kijamii hata kufikia kukifanya chama cha soka cha Hispania kuuhamisha mchezo wa kirafiki wa Novemba 13 kutoka Santiago Bernabeu kwenda Alicante kwa ajili ya kutuliza hali ya mambo.
0 comments:
Post a Comment