Barcelona,Hispania.
Wayne Rooney ameendelea kupongezwa baada ya hapo juzi kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa England baada ya kufikisha mabao 50 na kuipiku rekodi ya miaka 45 ya mabao 49 ya nyota wa zamani wa taifa hilo Sir Bobby Charlton.
Pongezi za hivi karibuni kwa Wayne Rooney zimetoka kwa mchezaji bora wa mwaka wa Ulaya Muargentina Lionel Messi ambaye amemwagia sifa Rooney na kusema " Wayne Rooney ni mchezaji bora wa kizazi hiki. Mmoja kati ya wachezaji spesho,ambaye huwezi kumlinganisha na yoyote.
“Kuna wachezaji wengi spesho,lakini Rooney ana ubora wa kipekee,ufundi na ana nguvu sana kuliko wachezaji wengi niliowahi kukutana nao,mwenye kujituma sana hakuna kama yeye.”
0 comments:
Post a Comment