Milan,Italia.
Imekuwa ni nadra sana kwa Mario Balotelli kuandikwa ama kusikika kwa mazuri kwenye vyombo vya habari.Siyo kwamba nyota huyu wa AC Milan hafanyi mazuri la hasha bali ni kuwa kwake mabaya yamekuwa ni mengi kuliko kawaida.
Wakati Mario Balotelli anarejea tena AC Milan kwa mkopo akitokea Liverpool wiki mbili zilizopita aliahidi kuacha utoto na utukutu wote na kuionyesha dunia kuwa yeye ni mkali katika kusukuma gozi la ng'ombe.
Lakini hayo yote ni kama yalikuwa danganya toto tu kwani tayari nyota huyo amejikuta matatani baada ya kupokonywa leseni yake ya udereva kufuatia kukiuka sheria za barabarani baada ya kuendesha gari lake la kifahari la Lamborghin kwa kasi ya zaidi ya 90kmph badala ya 50kmph kiwango ambacho kimepangwa kwa mtu kuendesha gari lake katika maeneo yenye makazi ya watu.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni huko katika jiji la Brescia alikozaliwa nyota huyo na kuibua maswali mengi ikiwa AC Milan ataachana na nyota huyo ama la kwani moja kati ya kipengere cha uhamisho kinasema Balotelli ahakikishe haingii katika matatizo nje na ndani ya uwanja.

0 comments:
Post a Comment