728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 08, 2015

    TUMECHOKA:MASHABIKI UFARANSA WAMKOMESHA OLIVER GIROUD

    Paris,Ufaransa.

    Kama ulidhani kuwa mshambuliaji Olivier Giroud anachukiwa na mashabiki wa Arsenal pekee basi sikia hii.

    Jana jumatatu kulikuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kimataifa kati ya Ufaransa na Serbia,Giroud akaanza kuharibu kama ilivyo kawaida yake.Mara ya kwanza mashabiki wakamsamehe ya pili wakamsamehe ya tatu uzalendo ukawashinda wakaanza kumzomea kila alipokuwa akigusa mpira.

    Baada ya zomea zomea kuzidi huku Giroud nae akiendelea kuonyesha kiwango kibovu kocha wa Ufaransa Didier Deschamps hawakuwa na msaada zaidi ya kumuita benchi nyota huyo wa Arsenal na nafasi yake kuchukuliwa na Antoine Griezman dakika ya 60.

    Mpaka mwisho wa mchezo huo Ufaransa iliiibuka kidedea kwa mabao 2-1,mabao ya Ufaransa yalifungwa na Blaise Matuidi huku lile la kufutia machozi la Serbia likifungwa na Aleksandar Mitrovic.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TUMECHOKA:MASHABIKI UFARANSA WAMKOMESHA OLIVER GIROUD Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top