728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 07, 2015

    TAMBWE AVUJISHA SIRI ZA MAVUGO


    MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe, amesema ingekuwa ni vigumu kwa mchezaji Laudit Mavugo kung’ara katika Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kama angesajiliwa na Simba kutokana na aina ya uchezaji wake wa kuvizia.

    Tambwe  kuwa anamfahamu vyema Mavugo kutokana na uwezo wa kuzifumania nyavu, lakini kutokana na aina ya soka la hapa nchini linalohitaji nguvu na kupambana hasa, ingekuwa vigumu kwa mdungaji huyo hatari wa Vital’O ya Burundi kung’ara hapa nchini.

    Alisema Mavugo ni mzuri zaidi akiwa na mpira na ana shabaha ya kufunga, lakini si mshambuliaji wa kuhangaika na kutafuta mipira au kupokea mipira, zaidi ya kuwa mtu wa kusubiri kutafuniwa na kufunga mabao akiwa hapendi taabu uwanjani wala kujishughulisha.


    Mavugo sio mbaya, ni mchezaji mzuri sana, lakini tatizo yeye hapendi shida, ni mtu wa kutafuniwa na kufunga mabao, ingekuwa ngumu sana mashabiki na wapenzi wa soka hapa nchini kumuelewa aina yake ya uchezaji, endapo Simba wangemsajili wangemuona hafai,” alisema Tambwe.

    (BINGWA)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TAMBWE AVUJISHA SIRI ZA MAVUGO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top