728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 07, 2015

    PRE-SEASON YAZUA MAMBO:SHABIKI CHELSEA ALIA NA WANAOWAPONDA NYOTA WAO

       George James
       (Shabiki Chelsea,Iringa)
                       
                         

    Mi nawashangaa sana watu wa humu ndani, binafsi sikupenda ujio wa Falcao(huyu wa sasa) ila kocha ndiye anayejua zaidi.Ninachoshangaa ni kuona kila tukicheza mechi na tukapoteza basi lawama zinawaangukia Begovic, Ramires, Cuardrado au Falcao.
                                 Asmir Begovic
    Mi nnaamini hakuna hata goli moja tulilofungwa ktk preaseason hii kwa uzembe wa Kipa ila ni Makosa ya kawaida ya  Beki zetu.Sitaki kufafanua zaidi hilo ila ingia youtube kuzicheki.
    Kwamaana hiyo Begovic au Courtois hapo mtakuwa mnamuonea.

    Kumbukeni Begovic ni kipa namba 2 (ingawaje anavaa 1 mgongoni). Na yule anayesema  bora kuwa na Cech kuliko hawa waliokuwepo huyo hajitambui kiakili.Huwezi kuwa na makipa wawili wenye uwezo wa dunia ktk timu moja.Hata Arsenal wamekubali kumruhusu Schezny  c kwasababu ni mbaya La hasha, bali ni kutokana na Schezny ana malengo ya kufika kiwango alichofika Cech kimafanikio. Hivyobasi akiendelea kubaki Arsenal ataishia kuwa kipa wa kawaida tu na siyo kipa tegemezi wa Taifa lake kama ilivyo kwa Cech.

    Ushahidi juu ya hoja yangu hiyo ni kwamba Kaulize hata Google kama kuna klabu yoyote Duniani yenye makipa wawili wenye level ya Dunia na wakawa timu moja, HAKUNA.
    Tuje kwa Ramires.Haina maana kuwa nnamtetea huyu jamaa lkn penye ukweli wacha tuuseme hata kama utawaumiza.

    Mechi zote tulizofungwa ktk preaseson na Ngao ya Jamii Ramires HAKUCHEZA DAKIKA 90.
    ukiangalia kwa umakini m, karibu magoli yote yaliyofungwa hayakuhusiana na Uzembe wa Ramires.
    Najua ataibuka mtu na kusema YEYE SI NDIYO KIUNGO MKABAJI, lengo lake ni kumsukumia gunia la misumari Ramires kwakuwa tu HAMPENDI.
    Naomba mtu ajenge hoja kumuhusu Ramires, lkn mi naamni hatukufungwa kwakuwa Rami amecheza chini ya Kiwango bali kwa makosa ya beki zetu.
    Kama tulifungwa kwa Floppy ya Ramires basi wapi tulishinda kwa Activeness ya asiyekuwa Rami ktk defencive midfilder?Jengeni hoja kuwa BAADA YA KUTOKA RAMIRES TIMU ILIAMKA NA KURUDISHA GOLI, wapi?

    Nimalizie kwa Falcao.
     
    Niambieni nyie mlioangalia mechi za preaseason msimu huu, Je ni mechi ipi Falcao alipata pasi ambayo Straker wa kiwango cha dunia huwa ni nadra sana kukosa bao?Nilivyoona mimi siyo Diego Costa alipewa zaidi ya nafasi 3 ktk mechi tofauti za yeye na kipa au na beki mmoja tu na akakosa kufunga?Nendenj youtube mkaangalie magoli ya kizembe aliyoyakosa.

    Jana tu, tumemshuhudia Remi naye anakosa goli la yeye na beki mmoja na kipa tu na akapiga nje.
    Nikuulizeni nyie wazee wa lawama.Niambieni mechi moja tu ambayo Falcao alipata nafasi ya yeye na kipa tu au bekimmoja na kipa. A akakosa kufunga.Kapewa pasi ngapi za mwisho na akakosa goli?
    Je mnataka aushike mpira mikononi na aungize golini ndo mmuone?Ndiyo kusema hajui kujiposition  kiasi hazipati hizo nafasi?

    Nimemaliza
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PRE-SEASON YAZUA MAMBO:SHABIKI CHELSEA ALIA NA WANAOWAPONDA NYOTA WAO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top