728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 07, 2015

    HII HAPA BARUA YA WAZI YA DI MARIA KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED MARA BAADA YA KUTUA PSG


    Naandika barua hii kuishukuru familia nzima ya Manchester United kwa kuniunga mkono kwa mwaka mmoja niliokuwa sehemu ya klabu.
    Manchester United waliponichagua kuwa sehemu ya timu yao, nilijisikia kuheshimiwa kwasababu nilijua klabu hii ina maanisha nini na jinsi gani iliniamini.
    Hata hivyo, nafahamu mambo hayakwenda vizuri kama tulivyotarajia, naomba msamaha kwa hilo.
    Katika maisha ya mcheza mpira, kuna wakati mwingine mambo usiyotarajia na usiyoyataka yanatokea.
                                 Embedded image permalink
    Nawahakikishia kwamba haikuwa kujaribu. Nilijitahidi niwezavyo, lakini mpira sio kama hesabu: Mara zote kuna vitu vingi vinavyoathiri vile unavyofikiria.
     http://media.fyre.co/P9FVeHZhSuiuZ9gRa5o1_letter.PNG
    Samahani sana kwasababu sikufanya kile nilichotarajia katika klabu hii kubwa na ya ajabu.
    Natoa shukurani za pekee kwa bodi ya wakurugenzi na utawala ya Manchester United, vilevile kila kiongozi na wachezaji wenzangu walioniunga mkono.
    Pia shukurani za pekee ziwaendee mashabiki ambao mara zote waliniamini na kuonesha heshima na mapenzi makubwa.
    Sasa ni wakati wa kujiunga na PSG, lakini Utukufu wa Manchester United utabaki kwenye kumbukumbu zangu daima.
    Nawatakia kila la kheri
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HII HAPA BARUA YA WAZI YA DI MARIA KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED MARA BAADA YA KUTUA PSG Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top