Lagos,Nigeria
Kiungo wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Cote d' Ivoire ametwaa tena tuzo ya mchezaji bora wa Africa katika hafla iliyofanyika huko Lagos Nigeria usiku wa jana (alhamisi).
Toure aliwashinda Vincent Enyeama wa klabu ya Lille/Nigeria na Pierre Emerik Aubameyang wa klabu ya Borrussia Dortmund/Gabon kutwaa tuzo hiyo ambayo ni ya nne mfululilo.
Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na raisi wa chama cha
soka cha Africa (CAF) Alhaji Issa Hayatou na gavana wa jimbo la Delta , Dr Emmanuel Uduaghan katika hoteli ya Eko jijini Lagos,Toure amemshukuru Mungu,CAF pamoja na wote waliompigia kura.
Tuzo zote ni kama ifuatavyo...
Mchezaji bora Africa wa kiume Yaya Toure (Cote d’Ivoire na Manchester City)
Mchezaji bora wa ndani ya Africa Ndombe Mubele (DR Congo na AS Vita)
Mchezaji bora wa kike Asisat Oshoala (Nigeria na Rivers Angels)
Mchezaji bora anayechipukia Asisat Oshoala (Nigeria na Rivers Angels)
Mchezaji mwenye kipaji maridhawa Yacine Brahimi (Algeria na FC Porto)
Kocha bora wa mwaka Kheireddine Madoui (ES Setif)
Timu bora ya taifa ya wanaume Algeria
Timu bora ya taifa ya wanawake Nigeria
Klabu bora ya mwaka ES Setif
Mwamuzi bora wa mwaka Papa Bakary Gassama (Gambia)
0 comments:
Post a Comment