Milan,Italia.
Mshambuliaji Lukas Podolski 29 ameendelea kumtolea uvivu kocha wake wa zamani katika klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger na kudai kocha huyo alimkosea heshima.
Podolski ambaye mapema wiki hii alitua Inter Milan kwa mkopo akitokea Arsenal amesema licha ya kocha kutompa nafasi ya kucheza mara kwa mara lakini pia alishindwa hata
kumwambia kwaheri wakati anajiandaa kutua Milan.
Podolski amesema "Hakuniambia chochote.Hakunipigia simu wala hakusema kwaheri.Sihitaji maua wala busu toka kwake.
"Lakini ni kuhusu heshima,kuhusu kusema kwaheri.Kwangu heshima ni kitu muhimu.Sijui,labda alikuwa na tatizo jingine na mimi"
0 comments:
Post a Comment