Barcelona,Hispania.
Hali ya mambo ndani ya klabu ya Barcelona imeendelea kuchukua sura mpya kila inapoitwa leo.
Kama walivyosema wahenga kuwa ngoma ikivuma sana ikavuma weee mwisho hupasuka.
Hivyo dakika yoyote na muda wowote klabu ya Barcelona huenda ikaamua kuachana na kocha wake Luis Enrique na nafasi hiyo kupewa mwingine.
Habari za kuaminika toka ndani ya klabu hiyo na kuthibitishwa na kituo cha televisheni cha Catalunya habari zinasema jana usiku kulikuwa
na kikao kizito kati ya raisi wa klabu hiyo Jose Maria Batromeu na nyota Lionel Messi.
Agenda kubwa ilikuwa ni kujadili nini cha kufanywa ili kutuliza hali ya mambo klabuni hapo kufuatia mgogoro uliopo kati ya nyota huyo na kocha Luis Enrique.
Inasemekana kutokana na maelewano mabovu kati ya kocha huyo na wachezaji Batromeu amemtamkia Messi kuwa yuko upande wake na kuwa atamfuta kazi kocha huyo muda wowote kuanzia sasa na tayari jitihada za kumpata kocha mpya zimeshaanza.
Kati ya makocha wanaopigiwa chepuo ni Oscar Garcia nyota wa zamani wa klabu hiyo na kocha wa klabu ya Brighton ambaye hivi karibuni amekataa nafasi ya ukurugenzi wa michezo klabuni hapo baada ya kutimuliwa kwa Andoni Zubizarreta.
Jina jingine lililoibuka katika kikao hicho ni la kocha wa zamani wa klabu hiyo Frank Rijkaard ambaye huyu ni pendekezo la Messi mwenyewe.
0 comments:
Post a Comment