Barcelona,Hispania.
Kocha msaidizi wa zamani wa klabu ya Barcelona Muholanzi Henk ten Cate ameibuka na kusema kinachofanya mpaka leo Messi awepo klabuni hapo ni ahadi aliyoiweka kwa marehemu Tito Villanova vinginevyo angeshaondoka siku nyingi.
Cate amesema Messi alikwenda hospitalini kumjulia hali Villanova aliyekuwa akipambana na ugonjwa wa kansa wakati huo na kumuahidi kuwa hatohama Barcelona.
Lakini Cate ameongeza kuwa iwapo Messi atafanikiwa kuhama basi uhamisho huo utakuwa na faidi pande zote mbili kwake na kwa klabu.
Amesema "Messi amekuwa Barcelona kwa kipindi kirefu sasa
nafikiri muda umefika anapaswa kuondoka na kuangalia maisha kwingine.
Bado ana thamani kubwa ya pesa ambayo muda siyo mrefu itashuka.
"Amekuwa katika dunia ya peke yake kwa miaka 10 mfululizo lakini sina hakika kama atarejea tena kwenye kiwango tulichokizoea
"Siyo kawaida kwa mchezaji kuwa juu kwa miaka 10 kama alivyofanya Messi.Nyota wengi wamekuwa wakidumu kwa miaka saba au nane na kisha kupotea.
Nikiongea ukweli bila kupepesa macho msimu uliopita Messi hakuwa vizuri japo takwimu zake zilimbeba"
0 comments:
Post a Comment