London,England.
SIKU za mshambuliaji mtukutu,Diego Costa klabuni Chelsea sasa ni kama zinahesabika hivi hii ni baada ya kuripotiwa kuwa tayari amesaini mkataba wa awali na klabu ya Tianjian Quanjian inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini China.
Habari kutoka nchini Hispania kupitia Cadena SER, zimasema kuwa Ijumaa iliyopita Costa akiwa na wakala wake, Jorge Mendes walikutana na maafisa wanne wa klabu ya Tianjin Quanjian kwenye mgahawa mmoja uliopo jijini London na kufikia makubaliano yaliyopelekea kusainiwa kwa mkataba huo wa awali.
Kupitia mkataba huo Costa mwenye umri wa miaka 28 atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni Milioni 25.3 kwa mwaka na kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa wakilipwa mkwanja mrefu zaidi kwenye ligi kuu ya soka nchini China.
Habari zaidi zinasema baada ya maafisa wa Tianjian Quanjian kufanikiwa kumsainisha mkataba huo Costa, baadae mwezi huu watakutana na uongozi wa Chelsea ambapo wataweka mezani ofa yao ya Pauni Milioni 76 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo mzaliwa wa nchini Brazil.
Ikumbukwe mwezi Januari mwaka huu Chelsea iliikataa ofa ya Pauni Milioni 80 iliyoletwa na Tianjian Quanjian kwa ajili ya kumsajili Costa.
0 comments:
Post a Comment