Faridi Miraji , Dar es salaam.
Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amelitaka shirikisho la soka nchini TFF kujikita katika kuhakikisha kuwa inakuza viwango timu ya Taifa katika viwango vya FIFA badala ya kupoteza Muda kwenye vikao vya kuwafungia wadau wa soka. Akifafanua , Chumi alisema mpaka Machi mwaka huu, Tanzania ilikuwa nafasi ya 157 wakati Taifa kama Afghanistan ambao wako vitani Muda wote walikuwa nafasi ya 156.
'"Ili kupanda katika viwango vya FIFA lazima timu ya Taifa icheze mechi za kutosha ambazo ziko kwenye kalenda ya Fifa, Sasa kwa mfano mwaka 2016 tumecheza mechi tatu ukilinganisha na majirani zetu Rwanda mechi 11, Uganda 13, Kenya 10 Afghanistan mechi 6" Alisisitiza Chumi
Akisisitiza zaidi, Mbunge huyo mwanamichezo alifafanua kuwa katika kipindi cha miaka mitatu toka 2014-2016 Taifa Stars ilicheza mechi 24 tu kulinganisha na mechi 47 wakati wa miaka mitatu ya mwisho ya Uongozi wa Leodgar Tenga 2011-2013.
'Ndio mana watu wanamkumbuka Tenga '.
Chumi aliongeza kuwa bila kupandisha viwango vya Fifa, Tanzania itaishia kuangalia AFCON na Kombe la Dunia kwenye luninga.
"Kupandisha viwango kunasaidia kukwepa kupangwa na timu vigogo, na Ndio mana kila mwaka tunajikuta katika hatua za awali tu tunapangiwa na Vigogo , mfano tulipowatoa Malawi tunajikuta tunaangukia kwa Algeria".
Mbunge huyo alisema kuwa kuthibitisha kuwa kushiriki mechi zilizoko kwenye Kalenda ya Fifa kunasaidia kupandisha viwango, takwimu zilizotolewa Jana tarehe 4 April 2017 na FIFA , Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 157 mpaka ya 135 baada ya kucheza na Burundi na Botswana.
Kufungia wadau bila kuwasikiliza sio Sawa , mwaka Jana Kufuatia sakata la kupanga matokeo ligi daraja la kwanza, baadhi ya wachezaji walifungiwa miaka kumi.
''Katika soka kumfungia mchezaji miaka kumi ni kumumaliza, Hata Ulaya maximum mtu anacheza ni miaka kumi, Sasa unamfungia mchezaji miaka kumi, kweli ndo mana hii ni Tanzania Football Fungiafungia '
Pamoja na TFF ambayo Chumi aliita ni Tanzania Football Fungiafungia kutokana na tabia ya hivi karibuni ya kuwafungia wadau wa soka, alivishukia Vilabu vya soka vya Simba na Yanga kuwa viongozi wake wajitazame haiwezekani mpaka Sasa havina viwanja.
Kauli ya Chumi inakuja baada ya TFF kuwafungia Wadau wakubwa michezo wengine hata bila kuwasikiliza ilimfungia kipa Wao Simba Dennis Richard miaka kumi aliyekuwa anacheza Geita Gold mine Kwa mkopo kwa kosa la kupoteza muda baada ya kwenda chooni dakika kumi ikitafasiliwa Kama upangaji wa matokeo, Ingawa adhabu yake ilifutwa, mdau mwingine aliyefungiwa ni Dumbaro yeye alifungiwa miaka saba baada ya kutaka kuzitetea vilabu kuhusu maslai yao, mkasa huu ulimkumba msemaji wa Yanga Jerry Murro Kwa kosa la kuisema ovyo tff yeye alifungiwa mwaka mmoja adhabu yake inaisha June mwaka huu, pia sakata TFF Fungia fungia ikampiga kitanzi Msemaji wa Simba hajji Manara mwaka mmoja na Milioni tisa kwa makosa matatu.
'Unajiita Rais wa Klabu, je unaacha legacy gani, unajiita Rais wa Yanga, Rais wa Simba timu inategemea uwanja wa mazoezi wa Boko Veteran, wajitazame.
SOKA LETU SASA LIWE LA KULIPWA.
Akizungumzia soka yetu, Chumi alimtaka Waziri Kuja na mkakati wa kuifanya soka yetu kuwa ya kulipwa Ili Serikali ijipatie mapato.
Soka ni biashara, angalia EPL pamoja na kuwa Timu Yao ya Taifa haiko vizuri lakini soka yao ni biashara kubwa duniani, michezo ni biashara.
0 comments:
Post a Comment