Farid Miraji,Dar Es Salaam.
Baada ya juzi Jumatano, Rais wa Simba, Evans Aveva kutangaza klabu hiyo ina mkataba na mshambuliaji wa Kagera Sugar, Mbaraka Yusuph anayeitumikia klabu ya Kagera Sugar, straika huyo ameibuka na kumkana kiongozi huyo kwa kuweka wazi kuwa hana mkataba na timu hiyo.
"Wao wenyewe viongozi wa Simba wanatambua kwamba mimi siyo mchezaji wao kwa sababu nilishamalizana nao tangu msimu uliopita na nacheza Kagera Sugar nikiwa mchezaji halali kabisa kwa ajili ya timu hiyo.
"Kama wao Simba wana uthibitisho kwamba nina mkataba wao na mimi nitawaonyesha mkataba wangu ambao unanionyesha kwamba nipo huru kwa ajili ya kuitumikia timu yangu ya sasa,"
Alipoulizwa kuhusu kadi ya usajili ambayo Aveva allionyesha kwa waandishi wa habari juzi, ikiwa na jina la Mbaraka Yusuph akitambulishwa kama mchezaji wa Simba, Mbaraka alisema:
"Kadi ile ni ya U-20, wakati huo nilikuwa naichezea Simba kabla ya kupelekwa kwa mkopo Kagera, muda wake ulishaisha, nikasaini mkataba Kagera Sugar ambao unaisha mwishoni mwa msimu."
0 comments:
Post a Comment