728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 05, 2017

    Kauli ya Kagera Sugar baada ya Simba kudai Mbaraka Yusuph ni mchezaji wao halali


    Kagera,Tanzania.

    UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa mshambuliaji Mbaraka Yusuph ni mchezaji wao halali kwa sababu alikamilisha taratibu zote za usajili wa kuitumikia klabu hiyo.

    Kauli hiyo imekuja kufuatia juzi Rais wa Simba, Evans Aveva, kusema kuwa Mbaraka ni mchezaji wao halali na wanayo leseni ya kuichezea timu yao katika msimu wa mwaka 2016/17.


    Akizungumza jana, Meneja wa Kagera Sugar, Mohammed Hussein, alisema kuwa Simba wanatakiwa waangalie walipokosea lakini kuhusiana na mshambuliaji huyo wao walimsajili kihalali na kupata leseni ya kumtumia.Hussein alisema kuwa wanawataka Simba kuangalia na kuthibitisha majina ya mchezaji huyo ambaye kwa sasa kiwango chake kimeimarika na kumfanya Kocha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) Salum Mayanga amwite kwenye kikosi chake.


    "Mbaraka ni mchezaji wetu halali, tulifuata na kukamilisha taratibu zote za usajili. Huyu mchezaji anaitwa Mbaraka Yusuph Abeid,lakini kwenye leseni ya Simba inaonyesha anaitwa Mbaraka Abeid, wakamtafute huyo mchezaji," alisema Hussein.


    Aliongeza kuwa anaishauri Simba kuwekeza nguvu kusaka ushindi katika mechi zake za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizosalia pamoja na mchezo wa fainali ya Kombe la FA badala ya kupoteza muda kwa mambo ya nje ya uwanja.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kauli ya Kagera Sugar baada ya Simba kudai Mbaraka Yusuph ni mchezaji wao halali Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top