Monaco,Ufaransa.
Juventus imeitoa nishai Monaco baada
ya usiku huu kuifunga mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya
nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya uliochezwa kwenye
dimba la Stade Louis II huko jijini Monaco nchini Ufaransa.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na
mwamuzi Lahoz kutoka Hispania ilishuhudiwa Juventus ambao walikuwa wageni
kwenye mchezo wa leo wakipata mabao yao katika kipindi cha kwanza na cha pili kupitia
kwa mshambuliaji wao wa kimataifa kutoka nchini Argentina,Gonzalo Higuaini aliyefunga
katika dakika za 29 na 59.Mabao yote yakitokana na krosi safi za mlinzi wa
kulia wa kimataifa kutoka Brazil,Dani Alves aliyekuwa akipanda mara kwa mara kusaidia
mashambulizi.
Ushindi huo muhimu umeiweka Juventus
katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo kwani katika
mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumanne ijayo huko jijini Turin nchini
Italia,miamba hiyo itahitaji matokeo ya ushindi wowote ama sare ili iweze
kukata tiketi ya kuelekea jijini Cardiff,Wales ambako bingwa wa michuano hiyo
atatafutwa.
0 comments:
Post a Comment