728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 19, 2017

    Hili ndilo eneo pekee ambalo ligi kuu bara imeizidi Bundesliga


    Munich,Ujerumani.

    WAKATI kwa sasa Tanzania siyo ishu tena kuona mwamuzi wa kike akipewa jukumu la kusimama kati na kuchezesha michezo mbalimbali ya ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ikiwemo hata ile ya watani wa jadi Simba na Yanga,nchini Ujerumani jambo hilo bado ni geni na halijawahi kutokea kabisa kwa mwanamke kuchezesha ligi ya Bundesliga lakini msimu ujao historian hiyo itafutwa na kuandikwa upya. 

    Ishu iko hivi kuanzia msimu ujao Mrembo,Bibiana Steinhaus atakuwa akichezesha michezo ya ligi ya Bundesliga na hivyo kuwa mwamuzi wa kwanza wa kike kuchezesha ligi hiyo ya juu kabisa nchini Ujerumani.

    Chama cha soka cha Ujerumani (DFB) kimetangaza kuwa Steinhaus ambaye mbali ya kupuliza kipyenga pia ni askari polisi atakuwa akisimama kati kuchezesha michezo mbalimbali ya ligi ya Bundesliga.

    Kabla ya kupewa shavu hilo kubwa na la maana,Steinhaus mwenye umri wa miaka 38 sasa alikuwa akichezesha ligi daraja la pili nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga 2 tangu mwaka 2007.



    Steinhaus amekuwa akitamba kwenye anga za kimataifa tangu mwaka 2005.Mwaka 2011 alichezesha fainali ya kombe la dunia la wanawake na mwaka 2012 alichezesha michuano ya soka ya Olimpiki.

    Juni 1 mwaka huu Steinhaus atakuwa kati kuchezesha mchezo wa fainali wa michuano ya klabu bingwa Ulaya kati ya timu za wanawake za Olympique Lyon na ndugu zao wa Paris Saint-Germain.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hili ndilo eneo pekee ambalo ligi kuu bara imeizidi Bundesliga Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top