Nice,Ufaransa.
OGC NICE ya Mario Balotelli imeitibulia Paris Saint Germain hesabu zake za kutwaa ubingwa wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa kwa mara ya pili mfululizo baada ya usiku wa kuamkia leo kuwafunga miamba hao mabao 3-1 katika mchezo mkali uliochezwa huko Allianz Riviera,mjini Nice.
Mario Balotelli ndiye aliyekuwa wa kwanza kutibua hesabu hizo baada ya kuifungia OGC Nice bao la kwanza ambalo lilifuatiwa na bao la pili ambalo lilifungwa na Mreno,Ricardo Pereira aliyetangazwa mchezaji bora wa mchezo huo.Bao la tatu limefungwa na Anastasios Donis.Bao la kufutia machozi la Paris Saint-Germain limefungwa na Marquinhos.
Aidha katika mchezo huo Paris Saint-Germain ililalizika kumaliza ikiwa na wachezaji tisa baada ya wachezaji wake wawili Thiago Motta na Angel Di Maria kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
Ushindi huo umeifanya OGC Nice ifikishe pointi 77 na kuendelea kubaki katika nafasi yake ya tatu nyuma ya Paris Saint-Germain yenye pointi 80 katika nafasi ya pili.Timu zote zimecheza michezo 35.Nafasi ya kwanza imekalia na AS Monaco yenye pointi 83 baada ya kushuka dimbani mara 34.
0 comments:
Post a Comment