728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, February 16, 2017

    Samatta agonga dakika tisini Genk ikilazimishwa sare Europa Ligi

    Giurgiu,Romania.

    KRC GENK inayochezewa na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania,Mbwana Samatta,imeshindwa kulinda ushindi wake mpaka mwisho na kujikuta ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Astra Giurgiu katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 32 bora ya michuano ya Europa Ligi uliochezwa usiku huu huko Arena Nationala,Romania.

    Genk ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza katika dakika ya 25 kupitia kwa Timoty Castagne.Bao hilo halikudumu sana kwani katika dakika ya 43 wenyeji walisawazisha kupitia kwa Constantin Budescu na kufanya mchezo uende mapumziko matokeo yakiwa sare ya bao 1-1.

    Kipindi cha pili walikuwa ni Genk tena walioanza kutikisa nyavu za wenyeji wao baada ya Leandro Trossard kufunga bao safi katika dakika ya 83 ya mchezo.

    Mchezo ukiwa unaelekea mwishoni Mjapan Takayuki Seto alizima ndoto ya Genk kuondoka na ushindi kwenye ardhi ya Romania baada ya kuisawazishia bao Astra Giurgiu  katika dakika ya 90 na kufanya mchezo uishe kwa sare ya mabao 2-2.





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Samatta agonga dakika tisini Genk ikilazimishwa sare Europa Ligi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top