Gent,Ubelgiji.
TOTTENHAM Hotspur imetolewa nishai huko Ghelamco Arena nchini Ubelgiji baada ya kukubali kichapo cha kushtua cha bao 1-0 kutoka kwa Gent kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 32 ya michuano ya Europa Ligi.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Jeremy Perbet katika dakika ya 59 akiunganisha krosi ya Danijel Milicevic na kumwacha kipa wa Tottenham Hotspur,Hugo Lloris akiwa hana la kufanya.
Katika mchezo mwingine Lyon ikiwa ugenini imeichapa AZ Alkmaar kwa mabao 4-1 kwa mabao ya Alexandre Lacazatte aliyefunga mara mbili,Lucas Tousart na Jordan Ferri.
Rostov imeifunga Sparta Prague kwa mabao 4-0 shukrani kwa mabao ya Miha Mevlja,Dmitriy Poloz, Christian Noboa na Sardar Azmoun.
Gustavo Blanco Leschuk ameipa Shakhtar ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Celta Vigo.Fiorentina imepata ushindi wa 1-0 dhidi ya Borussia Monchengladbach kwa bao la mkwaju wa faulo la Federico Bernardeschi.
0 comments:
Post a Comment