Dar Es Salaam,Tanzania.
MABAO mawili yaliyofungwa kipindi cha kwanza na cha pili na Mshambuliaji Ibrahim Ajib yameiwezesha Simba SC kuichapa AFC Leopards ya Kenya kwa jumla ya mabao 4-0 katika mchezo safi wa kimataifa wa kirafiki ulikokuwa maalumu kwa ajili kuadhimisha miaka themanini ya uhai wa klabu hiyo yenye makao yake makuu mitaa ya Msimbazi,Dar Es Salaam.
Simba SC ilianza kujihakikishia ushindi dakika ya 38 ya kipindi cha kwanza baada ya Ibrahim Ajib kufunga kwa mkwaju mkali wa mbali akimalizia pasi safi ya Mussa Ndusha.
Mpaka mapumziko Simba SC ilikuwa mbele kwa bao hilo moja huku wageni wao AFC Leopards wakiwa hawajapata kitu.
Kipindi cha pili Simba SC ilipata uhai zaidi baada ya kuwaingiza Jamali Mnyate,Laudit Mavugo kwani dakika ya 55 Ibrahim Ajibu aliifunga bao la pili baada ya kupokea pasi maridadi kutoka kwa Shiza Kichuya aliyekuwa mwiba mchungu kwa walinzi wa AFC Leopards
Dakika ya 66 Shiza Kichuya aliiandikia Simba SC bao la tatu akimalizia krosi ya Laudit Mavugo toka wingi ya kulia.Dakika ya 81Laudit Mavugo aliiandikia Simba SC bao la nne baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa wa AFC Leopards,Ivan Otieno uliotokana na mkwaju mkali wa winga wa kulia Shiza Kichuya.
Vikosi vilivyoanza
AFCLeopards XI: Bernard, Ian,Mwanzo, Wafula, Eugine, Joshua, Ongoma,Sozi, Ndirangu, Kiongera, Kiyai.
Simba XI: Angban, Hussein,Bokungu,Lufunga,Mwanjale, Ndusha, Mkude,Kazimoto, Blagnon, Ajib, Kichuya.
0 comments:
Post a Comment