728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 08, 2016

    ROBERTO MANCINI ATUPIWA VIRAGO INTER MILAN KISA BAO 6 ZA TOTTENHAM


    Milan,Italia.

    KLABU ya Inter Milan imetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu,Muitaliano Roberto Mancini na kumuajiri aliyekuwa kocha wa zamani wa Ajax,Mholanzi Frank De Boer.

    Taarifa kutoka nchini Italia zinasema kwa kipindi kirefu Mancini,51, amekuwa kwenye mvutano mkubwa kuhusu mambo mbalimbali na wamiliki wa klabu hiyo kampuni ya Suning Holdings Group ya China inayoongozaa na Rais wake Erick Thohir.

    Taarifa nyingine zinadai Inter Milan imeamua kuachana na Mancini baada ya klabu hiyo kufanya vibaya katika michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi ya Seria A.

    Ijumaa Inter Milan ilifungwa mabao 6-1 na Tottenham katika mchezo wa kimataifa wa kujipima nguvu.Kabla ya hapo ilifungwa na PSG kisha ikachapwa mabao 4-1 na Bayern Munich.

    Mancini alijiunga na Inter Milan miaka miwili iliyopita akitokea Manchester City na anatarajiwa kulipwa €2.5m kama fidia ya kuvunja mkataba wake ambao ulikuwa umebakiza mwaka mmoja ufike mwisho.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ROBERTO MANCINI ATUPIWA VIRAGO INTER MILAN KISA BAO 6 ZA TOTTENHAM Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top