728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 08, 2016

    MOURINHO AFICHUA SABABU YA KUMTOA MATA MUDA MFUPI BAADA YA KUMUINGIZA UWANJANI

    Manchester, England.

    KOCHA wa Manchester United,Mreno Jose Mourinho,amefichua sababu ya kumtoa kiungo wake Juan Mata muda mfupi baada ya kumuingiza uwanjani akitokea benchi katika mchezo ambao klabu yake ilitwaa ngao ya jamii kwa kuifunga Leceister City kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali wa ufunguzi wa ligi kuu England uliochezwa Jumapili jioni katika uwanja wa Wembley.

    Akiongea muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo,Mourinho,amesema hakumtoa Mata kwa sababu ya kuumia,kuchoka ama chuki dhidi yake bali ni kwa sababu za kiufundi.

    Mourinho amesisitiza kuwa aliamua kumtoa Mata na kumuingiza Henrik Mkhitaryan ili kukabiliana na mipira mirefu iliyokuwa ikitumiwa na wapinzani wake Leceister City ambao walikuja juu baada ya kufungwa bao la pili katika dakika za majeruhi.

    Amesema "Najua nimefanya kitu ambacho siyo kizuri kukifanya,kumtoa Mata.Sheria ziliruhusu kufanya mabadiliko (subs) sita na nilitaka kuusimamisha mchezo,kupoteza muda.

    Nilikuwa na mchezaji mmoja zaidi wa kumuingiza uwanjani hivyo ilinipasa kuchagua mchezaji mmoja mwenye umbo dogo zaidi ya wote atoke.Nikamtoa Mata.

    Baada ya kuwafunga bao la pili wapinzani wetu walianza kutumia mipira mirefu hivyo kwa kimo cha Mata ingetupa wakati mgumu sana kulinda ushindi wetu.Sikua na jinsi zaidi ya kumtoa na kumuingiza Mkhitaryan ambaye ni mrefu zaidi.

    "Lakini katika dakika chache alizokuwa uwanjani,Mata,alicheza vizuri,alinipa nilichokitaka.Alichukia nilipomtoa lakini baada ya kumwelewesha amenielewa na ana furaha tena".Alimaliza Mourinho.

    Mata aliingia uwanjani dakika ya 63 kuchukua nafasi ya Jesse Lingard,aliyekuwa ameumia baada ya kuchezewa faulo na kisha kutolewa dakika ya 88 na nafasi yake kuchukuliwa na Henrik Mkhitaryan.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MOURINHO AFICHUA SABABU YA KUMTOA MATA MUDA MFUPI BAADA YA KUMUINGIZA UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top