728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 08, 2016

    RASMI:THOMAS VERMAELEN AIHAMA BARCELONA NA KUJIUNGA NA AS ROMA


    Roma,Italia.

    MLINZI wa Ubelgiji,Thomas Vermaelen,rasmi ameihama Barcelona na kujiunga na AS Roma ya Italia kwa mkopo wa msimu mmoja wenye kipengele cha kununuliwa moja kwa moja.

    Vermaelen,30,ameihama Barcelona baada ya kufanikiwa kuichezea michezo 21 pekee katika kipindi cha misimu miwili alichohudumu katika klabu hiyo ya jimbo la Catalunya hii ni kutokana na kuwa majeruhi wa mara kwa mara.

    Akiongea na mtandao wa AS Roma baada ya kukamilisha uhamisho huo Vermaelen amesema anajisikia furaha kujiunga na klabu hiyo yenye makao yake makuu katika jiji la Roma.Pia amesema anajisikia furaha kucheza pamoja na nguli wa klabu hiyo,Fransesco Totti.

    Vermaelen alijiunga na Barcelona mwaka 2014 kwa dau la £15m akitokea Arsenal ambayo alijiunga nayo mwaka 2010 akitokea Ajax ya Uholanzi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RASMI:THOMAS VERMAELEN AIHAMA BARCELONA NA KUJIUNGA NA AS ROMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top