728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 09, 2016

    RASMI:PAUL POGBA AJIUNGA NA MANCHESTER UNITED KWA DAU LA REKODI YA DUNIA


    Manchester, England.

    MANCHESTER United imetangaza kupitia video fupi kumsajili kiungo wa Ufaransa,Paul Labile Pogba,kwa dau la rekodi la £89m ambalo ni kubwa zaidi kuwahi kutolewa katika mchezo wa soka.

    Pogba,23,amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia Manchester United baada ya kufaulu zoezi la upimaji wa afya yake lililofanyika Jumatatu jioni.

    Mkataba huo pia unampa Pogba nafasi ya kuongeza mwaka mmoja zaidi huku ukimuwezesha kuvuna kitita cha £300,000m kama mshahara wake wa wiki.

    Pogba amerejea Manchester United ikiwa ni miaka minne imepita tangu aihame klabu hiyo mwaka 2012 na kujiunga na Juventus kwa fidia ya £800,000m (€1.46m).




    Akiongea baada ya kukamilisha uhamisho huo Pogba amesema "Hii imekuwa ni klabu yenye sehemu maalumu katika moyo wangu na nina subiri kwa hamu kufanya kazi na Jose Mourinho.

    Pogba anakuwa mchezaji wa nne kujiunga na Manchester United tangu miamba hiyo ya Old Trafford ilipomuajiri Mreno Jose Mourinho kuwa kocha wake mpya.Wengine ni Eric Bailly,Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan.

    Akiwa na Juventus Pogba aliisaidia klabu hiyo ya jiji la Turin kutwaa mataji manne ya ligi ya Seria A na mawili ya Coppa Italia huku mwaka 2014/15 akiifikisha fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya na kuambulia kichapo cha mabao 3-1 toka kwa FC Barcelona.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RASMI:PAUL POGBA AJIUNGA NA MANCHESTER UNITED KWA DAU LA REKODI YA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top