728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 15, 2016

    BARCELONA YAIBAMIZA SEVILLA NA KUKARIBIA TAJI LA KWANZA HISPANIA


    Sevilla,Hispania.

    MABAO mawili ya kipindi cha pili ya Washambuliaji,Luis Suarez na Munir El Haddadi dakika za 54 na 81 yameipa Barcelona ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Sevilla katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa kuwania ubingwa wa Spanish Super Cup.

    Aidha Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Sanchez Pizjuan Stadium,Barcelona,ilipata pigo baada ya nyota wake wawili, Andres Iniesta na Jeremy Mathieu kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata majeruhi.

    Timu hizo zitarudiana tena Agosti 17 katika uwanja wa Camp Nou ambapo Barcelona itahitaji sare ama ushindi wowote ili kutwaa ubingwa huo wakati Sevilla wao watahitaji kuanzia mabao 3-0 ili waweze kuibuka mabingwa.

    Mchezo wa Spanish Super Cup huwa ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa ligi ya La Liga ni sawa na ngao ya jamii kwa England.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BARCELONA YAIBAMIZA SEVILLA NA KUKARIBIA TAJI LA KWANZA HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top