728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, July 04, 2016

    WESTHAM YAKIRI PAYET ANAWEZA KUTIMKIA BARCA,REAL MADRID

    London,England.

    MMLIKI Mwenza wa West Ham,David Gold,amekiri kwamba klabu yake inaweza kumpoteza staa wake,Mfaransa Dimitri Payet,ikiwa vilabu vya Barcelona ama Real Madrid vitamuhitaji.

    Gold ametoa kauli hiyo baada ya Payet,29, kuendelea kufanya vizuri katika michuano ya Euro na kuiwezesha timu yake ya Ufaransa imetinga hatua ya nusu fainali hali ambayo imeanza kuitia hofu klabu yake ya Westham kwamba huenda staa huyo akatwaliwa na vilabu vikubwa na tajiri zaidi yake.

    Gold amesisitiza kuwa West Ham imepania kumbakisha Payet wakati huu ambapo klabu hiyo inajiandaa kuhamia katika uwanja wake mpya wa Olyimpiki lakini amekiri kwamba itakuwa ngumu sana kumzuia staa huyo ikiwa atataka kujiunga na vilabu vya Barcelona ama Real Madrid.

    Gold ameliambia gazeti la The Sun "Tutapambana kadri ya uwezo wetu kuhakikisha Payet anavaa jezi za Westham msimu ujao.

    Tunataka kukiboresha kikosi chetu na Payet ni sehemu ya kile tunachotaka kukifanya.Lakini pia tunapaswa kuwa wakweli katika hili.Ikiwa Barcelona ama Real Madrid zitamuhitaji na yeye akahitaji kuhamia huko kwa kweli itakuwa ngumu sana kumbakisha.

    Huwezi kuwa na mchezaji mzuri na bora kama Payet halafu usitarajie kuona vilabu vikipigana vikumbo kumtaka.

    Mpaka sasa hatujapata simu yoyote kumhusu Payer,lakini naamini muda siyo mrefu zitaanza kuingia baada ya michuano ya Euro kuisha.Ngoja niwe mkweli,hatukaribishi simu yoyote kumhusu.

    Gold ameongeza kuwa West Ham haina tatizo la kifedha kwa sasa hata ilazimike kumuuza Payet.Gold amesisitiza hataki kuona klabu yake ikionekana ni duka la kuuza wachezaji japo biashara yoyote kumuhusu staa huyo mwenye mkataba mpaka mwaka 2021 itawaingizia faida kubwa.

    Wakati huohuo Gold amedokeza kuwa mpango wa klabu yake kwa sasa ni kusajili wachezaji bora ili iweze kupambana vyema na vilabu vya Chelsea, Arsenal, Manchester United ama Manchester City ambavyo kwao fedha/rasilimali siyo tatizo.

    Kwa sasa bado hatujawa na rasilimali za kutosha kuweza kupambao na vilabu hivyo kikamilifu lakini watu wanapaswa kutambua kuwa kwa sasa Westham siyo klabu ya kuuza wacheza bali ni klabu ya kufanya manunuzi makubwa ya wachezaji.






    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WESTHAM YAKIRI PAYET ANAWEZA KUTIMKIA BARCA,REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top