728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, July 04, 2016

    MLINZI LECEISTER CITY ADAI HAAMKI BILA KUIBUSU MEDALI YAKE YA UBINGWA WA EPL

    Accra,Ghana.

    MLINZI wa Ghana na Leicester City,Daniel
    Amartey,amesema hawezi kuamka asubuhi na kufanya mambo mengine bila ya kuibusu medali yake ya ubingwa wa Ligi Kuu England.

    Amartey,21,ambaye alijiunga na Leceister City mwezi Januari akitokea FC Copenhagen kwa ada ya £5m amefichua siri hiyo wakati akifanya mahojiano na kituo cha redio cha nyumbani kwao Ghana cha Starr FM.

    Amesema "Siamini kama mimi ni mshindi wa Ubingwa wa Ligi Kuu.Huwa naibusu Medali yangu kila asubuhi ninapoamka kutoka kitandani.Kuitwaa katika kipindi cha miezi sita pekee nilichokuwa na Leceister City imekuwa ni mafanikio makubwa sana".

    Msimu uliopita,Amartey, alifanikiwa kuichezea Leceister City michezo mitano ya ligi kuu na kuiwezesha klabu hiyo ya King Power kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa Ligi Kuu England baada ya kuusotea kwa miaka 132.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MLINZI LECEISTER CITY ADAI HAAMKI BILA KUIBUSU MEDALI YAKE YA UBINGWA WA EPL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top