728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, July 04, 2016

    CAF YAKUBALI KUBADILI TAREHE YA MCHEZO WA SHIRIKISHO KATI YA YANGA NA MEDEAMA

    Cairo,Misri.

    Shirikisho la Soka Barani Afrika limebadili tarehe ya mchezo wa Yanga dhidi ya Medeama wa kombe la shirikisho Afrika kutoka siku ya Ijumaa ya tarehe 15 Julai na sasa mchezo huo utachezwa Jumamosi ya tarehe 16 Julai katika uwanja wa taifa,jijini Dar es Salaam.

    CAF imefikia uamuzi huo baada ya Yanga kuomba kubadilishiwa tarehe ya mchezo wake dhidi ya Medeama.Awali ikumbukwe CAF waliwakatalia Yanga kubadili siku ya mchezo wa pambano lao dhidi ya TP Mazembe kwa kuwa walichelewa kuwasilisha ombi lao. 

    Kwa kulitambua hilo,Yanga walituma ombi lao mapema kuomba kubadilishwa kwa mchezo wao dhidi ya Medeama na CAF kuwakubalia hii leo.

    Pambano kuchezwa Jumamosi kutatoa fursa kwa Yanga kupata nguvu ya mashabiki zaidi kulinganisha na tarehe ya awali ya Ijumaa.

    Yanga iliyofungwa na TP Mazembe bao 1-0 katika mchezo uliopita na kujikuta wakiburuza mkia katika kundi A baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CAF YAKUBALI KUBADILI TAREHE YA MCHEZO WA SHIRIKISHO KATI YA YANGA NA MEDEAMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top