Lille,Ufaransa.
WALES imeendelea kufanya miujiza katika michuano ya Euro 2016 baada ya usiku huu kufanikiwa kufuzu nusu fainali kufuatia kuifunga Ubelgiji kwa mabao 3-1 katika mchezo mkali wa robo fainali uliochezwa katika uwanja wa Stade Pierre-Mauroy huko Lille.
Ubelgiji ndiyo ilikuwa ya kwanza kuichokoza Wales baada ya kiungo Rajda Nainggolan kufunga kwa mkwaju mkali wa mita 29 akimalizia pasi ya nahodha Eden Hazard.
Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Wales ambayo ilikuja juu na kuanza kufunga bao moja baada ya jingine ikitumia udhaifu wa safu ya ulinzi ya Ubelgiji ambayo leo iliwakosa Thomas Vermaelen anayetumikia adhabu na Jan Vertoghen anayeumwa na kujipatia mabao yake kupitia kwa Ashley Williams 30',Robison Kanu 55' na Sam Vokes 85'.
VIKOSI
Wales : Wayne Hennessey; James Chester, Ashley Williams, Ben Davies;
Chris Gunter, Joe Allen, Joe Ledley (Andy King 78'), Aaron Ramsey (James
Collins 90'), Neil Taylor; Gareth Bale; Hal Robson-Kanu (Sam Vokes 80')
Goals: Williams (30'),
Ubelgiji: Thibaut Courtois; Thomas Meunier, Toby Alderweireld, Jason Denayer, Jordan Lukaku (Dries Mertens 75'); Axel Witsel, Radja Nainggolan; Yannick Carrasco (Marouane Feillaini 46'), Kevin De Bruyne, Eden Hazard; Romelu Lukaku (Michy Batshuayi 83')
0 comments:
Post a Comment