London,England.
Muda wowote kuanzia sasa klabu ya Arsenal itatangaza kukamilisha usajili wa mlinzi wa kati wa England,Rob Holding,kutoka Bolton Wanderers kwa ada ya Paundi Milioni 2.5.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Bolton News ni kwamba Jana Jumatatu jioni Holding mwenye umri wa miaka 20 alifika katika Makao Makuu ya Klabu ya Arsenal,London Colney na kufanyiwa vipimo vya afya ambavyo alifuzu na anatarajiwa kusaini kandarasi ya muda mrefu ya kuichezea miamba hiyo ya Emirates.
Msimu uliopita Holding alifanikiwa kuichezea Bolton Wanderers michezo 26 na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo.
Aina ya Uchezaji
Holding anafanishwa kiuchezaji na walinzi wa zamani wa Arsenal,Tony Adams na Steve Bould.
0 comments:
Post a Comment