Dar es Salaam,Tanzania.
NYOTA wa Kimataifa ya Zimbabwe,Bruce Kangwa, ametua nchini jioni ya
leo tayari kabisa kufanya majaribio ya kujiunga na Klabu Bingwa ya Afrika
Mashariki na Kati Azam FC.
Kangwa anatokea kwa vinara wa Ligi Kuu nchini humo Highlanders FC na
mpaka sasa ligi hiyo ikiwa
mapumzikoni kufuatia kumaliza mzunguko wa kwanza, amefanikiwa
kuwa kileleni kwa ufungaji bora akiwa na mabao saba.
Mzimbabwe huyo ameshachezea timu
yake ya Taifa mechi 20 na mpaka sasa yupo kwenye kikosi hicho na anamudu kucheza nafasi tatu tofauti
uwanjani, beki wa kushoto, winga wa kushoto na mshambuliaji.
0 comments:
Post a Comment