Manchester, England.
MENEJA wa Manchester United,Mreno Jose Mourinho ametaja wachezaji wake watatu bora wa muda wote na kumwacha raia mwenzie wa Ureno,Cristiano Ronaldo,katika orodha hiyo.
Akijibu swali aliloulizwa na mtandao wa Daily Express baada ya kutakiwa kutaja nyota wake watatu bora wa muda wote,bila kusita wala kupepesa macho Mourinho amewataja Lionel Messi (Argentina),Edison Arantes Pele (Brazil) na Diego Maradona (Argentina).
Kauli hiyo ya Mourinho inakinzana na ile aliyoitoa mwaka 2013 wakati akiinoa Real Madrid,pale alipodai kuwa Ronaldo ni bora,bora zaidi ya wote.
Akinukuliwa na gazeti la The Mirror ,Mourinho alisema Nimemtazama Maradona mara kadhaa.Sikuwahi kumuona Pele lakini Ronaldo ni bora sana,bora zaidi ya wote.
0 comments:
Post a Comment