Dar es Salaam,Tanzania.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa 2016/17 inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake kuanzia Agosti 20 mwaka huu ambapo Agosti 17 itatanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga SC na Azam FC
Kwa ujumla Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/ 2017
itaanza Agosti 20,Simba SC wakifungua dimba na Ndanda FC Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, huku Azam wakiikaribisha African Lyon Uwanja wa
Azam Complex, Chamazi,
Dar es Salaam.
Mechi nyingine za ufunguzi zitakuwa kati ya Kagera Sugar na Mbeya City
Uwanja wa Kaitaba,Bukoba, Toto Africans na Mwadui FC Uwanja wa
CCM Kirumba, Mwanza,Stand United na Mbao FC Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga, Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting Uwanja wa Manungu, Turiani,
Morogoro na Majimaji na Prisons Uwanja wa Majimaji Songea.
Mabingwa wa Ligi hiyo,Yanga watafungua dimba na JKT Ruvu Agosti 31 badala ya Agosti 20/21 Uwanja wa Taifa kutokana na kukabiliwa na pambano la ugenini dhidi ya TP Mazembe Agosti 23.
RATIBA KAMILI IKO KAMA IFUATAVYO
0 comments:
Post a Comment