728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 19, 2016

    KOCHA MHISPANIA ASEMA JOHN BOCCO HANA KIWANGO CHA KUCHEZA AZAM FC

    Dar es Salaam,Tanzania.

    Kocha mpya wa Azam FC, raia wa Hispania Zeben Hernandez, amemkataa
    mshambuliaji wa kutumainiwa wa timu hiyo John Bocco, kwa kusema hana kiwango cha kuichezea timu hiyo.

    Taarifa ambazo Soka Extra, imezipata zimedai uongozi wa timu hiyo ukiongozwa na mmilikiwa wa timu Yousof Bakhresa,wanataka kukutana na kocha Harnandez, ili kuzungumzia swala la mchezaji huyo ikiwezekana aendelee kufanya naye kazi hivyo
    hivyo pengine anaweza kumbadilisha.

    “Hernandez amesema Bocco siyo mchezaji sahihi kwenye kikosi chake na ametuomba tumtafutie kazi nyingine lakini kwetu ni mchezaji mwenye mchango mkubwa kwenye timu kuanzia inapanda hadi tunabeba ubingwa wetu wa kwanza wa Ligi ya Vodacom na hata ubingwa wa Kombe la Kagame
    tuliochukua mwaka jana tutajaribu kuzungumza naye ili afanye naye kazi hivyo hivyo lakini kama atagoma ni vyema tukaangalia utaratibu wakumtafutia nafasi kiwandani,” amesema mmoja wa kiongozi wa karibu kwenye timu hiyo.

    Beki Erasto Nyoni ndiyo mchezaji wa kwanza kiwango chake kukubalika na kocha huyo aliyetua hivi karibuni kuchukua nafasi ya Stewart Hall, aliyeondoka huku Muingereza huyo na makocha wengine waliopita chaguo lao la kwanza kwenye ushambuliaji likiwa ni Bocco.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA MHISPANIA ASEMA JOHN BOCCO HANA KIWANGO CHA KUCHEZA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top