728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 05, 2016

    TAARIFA YA SAMATTA KUTAKIWA AS ROMA YA ITALIA,WAKALA ATOA KAULI

    Dar es Salaam,Tanzania.

    Wakati suala la mshambuliaji Mbwana
    Samatta kuwa njiani kutua AS Roma ya Italia likiendelea kusambaa mitandaoni,meneja wake amesema ni uzushi mtupu.

    Jamal Kisongo ambaye ni meneja na mlezi wa Samatta, amesema hakuna lolote kuhusiana na hilo na Samatta anaendelea na maandalizi katika kikosi chake cha KRC Genk kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.

    “Nimesikia pia, kuna watu kadhaa wameniuliza pia. Lakini ukweli ni hivi;Mbwana anaendelea na maandalizi ya Ligi Kuu Ubelgiji.

    “Hakuna lolote kuhusiana na Roma hadi sasa labda kama litakuja baadaye Mawakala wake wote wanalijua hilo.

    “Timu haiwezi ikafanya mawasiliano ya kumuuza bila ya kuwaeleza mawakala wake, meneja wake. Ndiyo maana nasema labda suala hilo lije baadaye,” alisema Kisongo.

    Kuanzia leo asubuhi, taarifa za AS Roma ya Italia imekuwa kwenye mazungumzo Genk namna ya kumnasa Samatta ambaye ni nahodha wa taifa Stars,zimekuwa zikisambaa kwa kasi.

    Chanzo:Saleh Ally.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TAARIFA YA SAMATTA KUTAKIWA AS ROMA YA ITALIA,WAKALA ATOA KAULI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top